Loading...

POSHY QUEEN: NISIFANANISHWE NA SANCHI, HATUFANANI

Loading...
Mrembo anayekimbiza kwenye Mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata Jackline Obeid maarufu kama Poshy Queen ameibuka kutaka asifananishwe na watu wengine.

Poshy amefunguka na kusema kuwa hataki kufananishwa na mrembo mwingine ambaye anatengeneza headlines kila siku kwa umbo lake matata anayejulikana Kama Sanchi.

Katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Sanchi amefunguka na kusema kwamba hataki kufananishwa na Sanchi kwani yeye binafsi haoni kama wamefanana.

"Naomba niweke hiki kitu ili kiwe clear sidhani kama ni sawa kunifananisha mimi na watu kwanza hatufanani, hatuna undugu sio marafiki na hata mtu akituangalia hatufanani kwanza hata shepu zetu hazifanani halafu mimi ni mrefu kwake kwaiyo hatuendani".

Sanchi na Poshy Queen wamekuwa wakifananishwa kutokana na wote wawili kuwa na maumbile makubwa Lakini pia wote wamekuwa wakiachia picha tata kwenye Mitandao ya kijamii.
Na Frank Daudi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
POSHY QUEEN: NISIFANANISHWE NA SANCHI, HATUFANANI POSHY QUEEN: NISIFANANISHWE NA SANCHI, HATUFANANI Reviewed by By News Reporter on 2/15/2019 05:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.