Loading...

MAREKANI: MKE AMUUA MUMEWE KWA SUMU ILI AOLEWE

Loading...
MWANAMKE mfanyakazi katika gereza kutoka Missouri, Marekani anatuhumiwa kuwa alimuua mumewe kwa kumtilia sumu kwenye chakula, ili waoane na mpenzi wake mfungwa.

Amy Murray, wa miaka 40 alishtakiwa Ijumaa kwa mauaji ya mumewe Joshua Murray wa miaka 37, ambaye alipatikana akiwa maiti mnamo Desemba 11.

Japo mwanamume huyo alipatikana kitandani akiwa maiti, ripoti ya upasuaji wa mwili wake ilionyesha kuwa alikufa kutokana na kutiliwa sumu, kabla ya mtoto kuwashwa ndani ya nyumba yake.

Ni hapo ambapo wachunguzi katika kesi hiyo walibaini kuwa Amy alikuwa akifanya kazi ya uuguzi katika jela ya Jefferson na alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfungwa Eugene Claypool, wa miaka 40.

Amy anasemekana kuanzisha moto huo kisha akaondoka nyumbani kwake na mwanawe mvulana na mbwa wawili.
Na George Owino.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAREKANI: MKE AMUUA MUMEWE KWA SUMU ILI AOLEWE MAREKANI: MKE AMUUA MUMEWE KWA SUMU ILI AOLEWE Reviewed by By News Reporter on 2/16/2019 10:06:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.