Loading...

MBUNGE ALIYEBAMBWA AKIIBA MKATE NCHINI SLOVENIA AJIUZULU

Loading...
Mbunge mmoja nchini Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu kama ‘sandwich’ katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo kumdharau. 

Darij Krajcic ameviambia vyombo vya habari nchini humo kwamba alipuuzwa na wafanyakazi wa duka hilo na walikua wakiendelea na shuguli zao bila ya kumhudumia.

Kulingana na ripoti ya BBC ya Ijumaa, Februari 15, hakujilakana awali ikiwa mwanasiasa huyo alikuwa amefanya kitendo hicho, na baadae baadhi ya wanachama walisisitiza ni lazima kulipa pesa za mkate huo.

Inafahamika kuwa, Krajcic aliomba msamaha na kusema kuwa anajutia kitendo alichokifanya na kimemtia aibu kubwa.

Mdahalo kuhusu kisa hicho, uliibuka na kusambaa baada ya Bwana Darij kuwaarifu wabunge wengine wakati wa mkutano wa kamati uliofanyika Jumatano, Februari 13.

''Nilisimama pale kwa dakika tatu, kabla wanihudumie," mbunge huyo mwenye umri wa miaka 54 alisimulia katika kituo kimoja cha runinga binafsi.

Taarifa ilisema kuwa wafanyakazi watatu wa duka hilo hawakugundua kama kulikuwapo na mteja kwa sababu walikuwa katika mazungumzo.

''Hakuna mtu yoyote aliyepiga kelele, wala kunifuata.'' alisema profesa huyo wa zamani. 

Baada ya kuwasimulia kisa chake, wabunge wenzake walicheka sana na kushangazwa na tukio hilo, lakini Alhamisi spika wa bunge hilo Brane Golubovic, alikemea vikali kitendo cha mbunge kuiba, na kusema kuwa ni kitendo kisichokubalika.

''Amechukua hatua za kuwajibika na kujiuzulu yeye mwenyewe," Golubovic aliviambia vyombo vya habari.
Na Vicky Bernard.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MBUNGE ALIYEBAMBWA AKIIBA MKATE NCHINI SLOVENIA AJIUZULU MBUNGE ALIYEBAMBWA AKIIBA MKATE NCHINI SLOVENIA AJIUZULU Reviewed by By News Reporter on 2/16/2019 09:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.