Loading...
Mbunifu maarufu wa mavazi dunia Karl Lagerfield aliyefariki dunia siku mbili zilizopita ametajwa kuacha utajiri usiopungua Bilioni 456 na mrithi pekee anatajwa kuwa paka Wake anayeitwa Choupette.
Karl ambaye alikuwa mbunifu wa mavazi katika kampuni za Gucci na Fendi, alifariki Jumanne asubuhi, na Kifo chake kimeombolezwa na watu maarufu katika tasnia ya mavazi, ikiwa ni pamoja na dizaina wa Italia, Donatella Versace.
“Leo dunia imempoteza mtu maarufu,” alisema mhariri mkuu wa jarida la Vogue, Anna Wintour. Tovuti ya Lagerfeld inaonyesha alizaliwa mwaka 1938 japokuwa watu wengi wanasema alizaliwa miaka mitano kabla ya hapo.
Imeelezwa kuwa, Paka aitwae Choupette mwenye umri wa miaka Saba, aliyekuwa akimilikiwa na Karl Lagerfeld, ndiye anatazamiwa kurithi utajiri wa Mkongwe huyo anayetajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Tsh. Bilioni 456, Paka Choupette amekuwa akilelewa kifahari na Karl.

Na Frank Kavikule.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MBUNIFU MAARUFU WA MAVAZI AMUACHIA PAKA WAKE URITHI WA MABILIONI
Reviewed by By News Reporter
on
2/21/2019 11:08:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: