Loading...

NYOTA WAWILI SIMBA KUIKOSA MECHI YA YANGA

Loading...
Ni suala la muda tu ndio kitu pekee kimebaki kabla ya kuchezwa mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba, itakayofanyika leo Jumamosi Februari 16, ambapo katika mchezo huo Simba inamkosa nyota wake ambaye amekuwa akiipa matokeo Simba kwenye mechi mbalimbali za karibuni.

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la Erasto Nyoni dhidi ya Yanga msimu uliopita.

Si mwingine ni winga Shiza Kichuya, ambaye tangu aliposajiliwa na Simba mwaka 2016 akitokea Mtibwa Sugar amekuwa chachu ya matokeo mazuri ya Simba katika pambano la watani wa jadi.

Akiwa katika msimu wake wa kwanza wa 2016/2017 ndani ya Simba, Kichuya alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza kwenye mchezo huo mkubwa barani Afrika. Bao lake lilikuwa la kusawazisha dakika ya 87 ambapo alifunga kupitia kona ya moja kwa moja,  baada ya Yanga kutangulia kwa bao la Amissi Tambwe dakika ya 26.

Februari 25, 2017 Kichuya pia alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 iliopata Simba dhidi ya Yanga hivyo kuendelea kuwa na bahati ya kufumania nyavu katika pambano la watani wa jadi.

Kichuya hakuishia hapo, Jumamosi ya Oktoba 28, 2017 aliifungia Simba bao la kuongoza dhidi ya Yanga dakika ya 58 lakini Yanga walisawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Obrey Chirwa.

Kichuya kwasasa hayupo tena msimbazi baada ya kusajiliwa na klabu ya Pharco FC ya Misri ambayo nayo imemtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Enppi FC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Misri.

Mchezaji mwingine ambaye bado haijawekwa wazi kuwa atakuwa sehemu ya mchezo huo ni Erasto Nyoni ambaye ametoka majeruhi. Nyoni ni muhimu kwa Simba ambapo naye ni miongoni mwa waliofunga mabao ya Simba dhidi ya Yanga hivi karibuni.

Beki huyo kiraka uwanjani, alifunga bao pekee lililoipa ushindi Simba dhidi ya Yanga April 29, 2018.

Kwa upande wa vinara wa mabao msimu huu kwa kila timu tayari Heritier Makambo wa Yanga ambaye ni raia wa DR Congo ana mabao 11 na ndio kinara wa wafungaji mpaka sasa huku kwa Simba Meddie Kagere anaongoza akiwa na mabao 8.
Na Frank Saidi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NYOTA WAWILI SIMBA KUIKOSA MECHI YA YANGA NYOTA WAWILI SIMBA KUIKOSA MECHI YA YANGA Reviewed by By News Reporter on 2/16/2019 08:15:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.