Loading...

OPERESHENI SAKA 'WAGANGA WA JADI' YAPAMBA MOTO

Loading...
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amesema mikoa yote nchini imeanza  operesheni  kali  dhidi ya   waganga wa  jadi wanaopiga ramli chonganishi  kwa sababu wamekuwa chanzo cha  mauaji ya watu  nchini.

IGP Sirro alitoa msimamo huo jana katika kijiji cha Nyamilangano, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wakati akizungumza na   watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na  viongozi wengine wa Wilaya ya Kahama.

Alisema hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari kwa kuwa tayari wamefanikiwa kuanza kudhibiti  mauaji  ya watoto katika mikoa ya Njombe na Simiyu.

Sirro alisema  Jeshi la Polisi  lilifanikiwa kudhibiti na kukomesha  mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino,  lakini kwa sasa yameanza kujitokeza mauaji ya watoto ambayo  yanatokana na  uchonganishi wa waganga wa jadi.

IGP alisema ni lazima wawasake na kuwachukulia hatua kali na kwamba suala la kupiga ramli chonganishi ni ushamba ambao umepitwa na wakati.
Na Simon Majubwa.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
OPERESHENI SAKA 'WAGANGA WA JADI' YAPAMBA MOTO OPERESHENI SAKA 'WAGANGA WA JADI' YAPAMBA MOTO Reviewed by By News Reporter on 2/21/2019 11:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.