Loading...

RAIA WA MAREKANI AFARIKI DUNIA KENDWA BAADA YA KUZAMA NA MAJI

Loading...
Marvin Vldimir Salazar raia wa Marekani miaka 21 amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati akiongelea baharini huko Kendwa Roks Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa huo Haji Abdalla Haji amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 6 na dakika 30 usiku wa kuamkia leo  wakati marehemu huyo akiogelea baharini.

Kamanda Haji amesema chanzo cha kifo hicho ni marehemu kutokuwa na uweledi wa kuogelea katika fukwe ya  bahari hiyo.

Kamanda Haji ametoa wito kwa  wamiliki wa Hoteli kuweka utaratibu wa kusaidia watu wanapokumbwa na tatizo lolote katika sehemu za ufukwe za bahari ili kuepusha vifo vinavyoweza kuepukika.

Wakati hayo yakijiri kamanda Haji amesema hali ya usalama katika mkoa huo ipo vizuri na jeshi la polisi  limejipanga kuendeleza doria  kudhibiti wanaovunja sheria za nchi kwa makusudi.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIA WA MAREKANI AFARIKI DUNIA KENDWA BAADA YA KUZAMA NA MAJI RAIA WA MAREKANI AFARIKI DUNIA KENDWA BAADA YA KUZAMA NA MAJI Reviewed by By News Reporter on 2/15/2019 07:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.