Loading...

WASANII 300 KUTEMBELEA UJENZI WA RELI YA KISASA

Loading...
Wasanii 300 kutoka katika makundi ya sanaa wanatarajiwa  kufanya ziara ya kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa kutoka jijini Dar es salaam mpaka Morogoro.

Akiongea na waandishi wa habari, kiongozi wa wasanii na mratibu wa safari hiyo bwana Steve Nyerere amesema kuwa safari hiyo itawahusisha wasanii wote wa muziki, bongo movies, wacheza mpira na kila kundi linalohusu sanaa na burudani.

Steve anasema kuwa safari hii ni moja ya matokeo chanya ya kikao chao kilichofanyika wiki iliyopita kati yao na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda. Safari hiyo inategemea kuanza asubuhi na kupitia maeneo yote ambapo reli hiyo inapita.
Na Peter Maswi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WASANII 300 KUTEMBELEA UJENZI WA RELI YA KISASA WASANII 300 KUTEMBELEA UJENZI WA RELI YA KISASA Reviewed by By News Reporter on 2/06/2019 09:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.