Loading...

DIMPOZ ASHANGAZWA NA MANENO YA STEVE NYERERE

Loading...
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa ameshangazwa na maneno ambayo Msanii Steve Nyerere alisema Juu yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku za nyuma na chombo kimoja cha habari, Steve Nyerere aliibuka na kusema Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Ommy Dimpoz amemjia juu Steve Nyerere juu ya kauli hiyo na kumtaka awe makini na maneno yake kwani hajawahi hata siku moja kumpigia simu na kumjulia hali hivyo asingeweza kujua afya yake.

"Muda mwingine tunapaswa tuzitumie vizuri hizi kamera, kama kuna kitu huna uhakika ni vizuri usikizungumze, ungeweza hata kunitafuta kwanza, ila mimi sina tatizo nae, alijikwaa tu".
Na Catherine Kayombo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DIMPOZ ASHANGAZWA NA MANENO YA STEVE NYERERE DIMPOZ ASHANGAZWA NA MANENO YA STEVE NYERERE Reviewed by By News Reporter on 2/06/2019 09:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.