Loading...

DAWA YA UKIMWI YAMTIA HATIANI MCHUNGAJI ZIMBABWE

Loading...
Mahakama nchini Zimbabwe imemlima faini ya dola 700 mchungaji mmoja mashuhuri nchini Zimbabwe baada ya kumkuta na hatia ya kudanganya kuwa ana dawa ya miti shamba inayotibu Ukimwi.

Walter Magaya ambaye hujiita Mtume mwenye miaka 35, awali alikiri mashtaka ya kuvunja sheria Udhibiti wa Dawa ya nchi hiyo kwa kuuza dawa ambazo hajithibitishwa.

Mwezi Oktoba mwaka jana, aliwaambia wafuasi wa kanisa lake kuwa dawa hiyo, iitwayo aguma, ina nguvu za kimiujiza zinazoweza kuangamiza virusi vya ukimwi kwa siku 14.

Serikali ya Zimbabwe ilisema kufanya hivyo ni uhalifu na polisi wakavamia ofisi zake.

Polisi walimkamata mwezi Novemba 2018, na kuzuia dawa hizo ambazo alisema zinawatibu watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Zimbabwe ni nchi ya sita ya kiafrika kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na maambukizi ya kasi ya virusi vya Ukimwi.

Takribani watu 1.3 walikuwa wanaishi na Ukimwi nchini humo mwa 2016 kulingana na taarifa zilizokusanywa na Umoja wa Mataifa.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DAWA YA UKIMWI YAMTIA HATIANI MCHUNGAJI ZIMBABWE DAWA YA UKIMWI YAMTIA HATIANI MCHUNGAJI ZIMBABWE Reviewed by By News Reporter on 2/06/2019 10:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.