Loading...
Watu 31 wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko kufuatia kimbunga Idai kilichoandamana na mvua kupiga mashariki mwa nchi ya Zimbabwe.
Serikali imesema hayo jana. Kimbunga Idai tayari kimesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 katika nchi za Msumbiji na Malawi.
Waziri wa habari wa Zimbabwe amesema kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuwa vifo vingi vilitokea katika mji wa Chimanimani.
Kimbunga hicho kiliharibu nyumba kadhaa na kuharibu madaraja yaliyoko mashariki mwa mkoa wa Manicaland unaopakana na Msumbiji.
Mbunge mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, maelfu ya watu wameathiriwa na mafuriko pamoja na ukosefu wa umeme.

Na Ummy Kitwana.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIMBUNGA 'IDAI' CHAZIDI KULETA MAAFA, 31 WAFARIKI
Reviewed by By News Reporter
on
3/17/2019 09:05:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: