Loading...

BINTI WA MIAKA 16 AJINYONGA KISA MAPENZI

Loading...
Migoro, Kenya. Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 16 ameripotiwa kujitia kitanzi baada ya mpenzi wake kumtumia ujumbe wa kutaka wawili hao waachane 

Violet Adhiambo ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyangubo alipatikana ndani ya nyumba yao Jumanne Aprili 9, akiwa na kamba shingoni.

Kulingana na taarifa za The standard, Adhiambo aliamua kujitoa uhai baada ya kugombana na mpenziwe aliyekatiza uhusiano wao wa kimapenzi kupitia ujumbe mfupi kwa simu. 

Baada ya kuupokea ujumbe huo, Adhiambo aliwaambia marafiki wake kwamba hangestahimili machungu ya kuishi bila mpenzi wake kwani alikuwa anampenda sana.

Majirani walisema walijawa na wasiwasi baada ya kusikia simu ikililia ndani ya nyumba yao bila mtu kuipokea, walipochungulia kwenye dirisha, waliona mwili wa marehemu ukininginia kwenye paa ya nyumba. 

"Alikuwa mchangamfu nilipomuacha nyumbani nikielekea kazini na hakuonyesha dalili zozote kwamba alikuwa na tataizo," Mama Adhiambo alisema.
Na Saidi Juma.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BINTI WA MIAKA 16 AJINYONGA KISA MAPENZI BINTI WA MIAKA 16 AJINYONGA KISA MAPENZI Reviewed by By News Reporter on 4/12/2019 08:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.