Loading...

MAN UTD YAPIGWA 4G, ARSENAL NAYO CHALII

Loading...
Klabu ya Manchester United jana wamechezea kichapo cha mabao 4-0  dhidi Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Engalnd uliochezwa kwenye  uwanja wa Goodison Park.

Magoli ya Everton yamefungwa na Richarlison dakika ya 13, Gylfi Sigurdsson dakika ya 28, Lucas Digne dakika ya 56 na Theo Walcott dakika ya 64.

Matokeo hayo yanaifanya Man United kuwa hatarini kuikosa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, kwani imesalia na pointi zake 64 katika nafasi ya sita.

Wakati United wakila kichapo hicho,  Arsenal imeangukia pua baada ya  kukubali kichapo cha magoli 3-2 kutoka kwa Crystal Palace katika mchezo uliochezwa Emirates nyumbani kwa Arsenal

Crystal Palace ndiyo walikua wa kwanza kupata bao kupitia kwa Christian Benteke dakika 17 kabla ya Mesut Ozil kusawazisha dakika ya 47.

Dakika ya 61 Wilfred Zaha akaiandikia Crystal Palace goli la pili kabla ya James McArthur kuandika goli la tatu dakika ya 69

Arsenal wakaendelea kujipapatua na dakika 81 Pierre Emerick Aubemeyang akaindikia Arsenal goli la 2 lakini wakashindwa kuchomoa goli la tatu na hatimae mchezo ukamalizika kwa Crystal Palace kushinda magoli 3-2

Kipigo cha Arsenal kimewafurahisha zaidi mashabiki wa Chelsea na Manchester United ambao wapo kwenye vita ya kuwania nafasi nne za juu ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabigwa barani Ulaya msimu ujao.

Kwa matokeo hayo Arsenal imesalia katika nafasi ya nne akiwa na point 66 akifuatiwa na Chelsea mwenye alama 66 pia katika nafasi ya tano wakati  Man United wapo nafasi ya sita wakiwa na point 64.

Kwingineko kwenye EPL, Liverpool bado imesimama imara kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo baada ya hii leo kumtandika Cardif City goli 2-0

Magoli ya Liverpool hii yamefungwa na Georginio Wijnaldum na James Milner aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

Kwa ushindhi huo Liverpool imerejea kileleni baada ya kufikisha point  88 wakimuacha Man City katika nafasi ya pili wakiwa na point 86 ingawa Man City anamchezo mmoja mkononi.
Na Christian Godfrey.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAN UTD YAPIGWA 4G, ARSENAL NAYO CHALII MAN UTD YAPIGWA 4G, ARSENAL NAYO CHALII Reviewed by By News Reporter on 4/22/2019 08:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.