Loading...

UCHAGUZI UKRAINE: MCHEKESHAJI ZELENSKY ASHINDA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS

Loading...
Mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais , kutokana na kura zilizopigwa.

Kura hizo zimempa nafasi mwanasiasa mpya ambaye amechaguliwa kwa kuungwa mkono na zaidi ya asilimia 70.

Bwana Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ameweza kumtoa madarakani rais Petro Poroshenko ambaye amekubali kushindwa.

Matokeo ya sasa yanaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa bwana Poroshenko na kukataliwa kuanzishwa kwa Ukraine mpya.

"Sitawaangusha ," Bwana Zelensky aliwaambia waliomuunga mkono wakati wa sherehe za kujipongeza.

Aliongeza kusema "Sijawa rais bado lakini kama raia wa Ukraine, ninaweza kuwaambia nchi zote za Kisovieti kuwa watuangalie sisi, Kila kitu kinawezekana !"

"Kama kura ziko sawa, basi atakuwa amechaguliwa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano". Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa hapo baadae.

Zelensky anajulikana kwa umahiri wa ucheshi wake kama muigizaji nyota wa mfululizo wa filamu ya satirical katika television ambapo anaigiza kama rais wa Ukraine.

Rais ana mamlaka makubwa katika upande wa usalama, jeshi na sera za kigeni katika nchi hiyo.

Volodymyr Zelensky ni nani?

Zelensky amekuwa akicheza mchezo wa kuigiza inayoitwa 'Servant of the People ' ambapo kwa bahati tu akawa muigizaji anayetaka kuwa rais wa Ukrainne.

Anacheza kama mwalimu ambaye aliyechaguliwa baaada ya kufukuzwa kwa kosa la rushwa kusambaa katika mitando ya kijamii.

Aligombea nafasi ya urais kwa jina la chama cha siasa ambacho ni sawa na kipindi chake cha televisheni.

Akiwa hana uzoefu wowote wa siasa ,wkampeni za Zelensky ziliangazia utofauti wake na wagombea wengine badala ya mawazo ya sera.

Awamu ya kwanza alishinda kwa asilimia zaidi ya 30 za kura ambapo zilikuwa ni mara mbili ya mpinzani wake Poroshenko ambaye alikuwa na asilimia 15.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UCHAGUZI UKRAINE: MCHEKESHAJI ZELENSKY ASHINDA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS UCHAGUZI UKRAINE: MCHEKESHAJI ZELENSKY ASHINDA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS Reviewed by By News Reporter on 4/22/2019 07:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.