Loading...
Kulingana na vyombo vya habari vya mitaa Mkurugenzi Mtendaji wa Matibabu wa Msumbiji, Hussen Issa, amesema kuwa kesi za ugonjwa wa kipindupindu zimekuwa zikiongezeka toka siku ya Alhamisi mpaka kufikia 139.
Ofisi ya kikanda ya Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Msumbiji limeandika katika mtandao wa Twitter kuwa kutambua kwa mlipuko wa kipindupindu kumesaidia kuuthibiti kwa haraka.
"Dawa 900,000 za chanjo ya kipindupindu zinatumwa Msumbiji kwa ajili ya kusadia katika hali hiyo ya dharura ," WHO imesema.
Kimbunga Idai kilisababisha maporomoko huko Beira mnamo Machi 14 na upepo wa kilomita 177 kwa saa, na kuua watu angalau 534 huko Msumbiji, kulingana na vyombo vya habari vya mitaa.
Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MILIPUKO YA KIPINDUPINDU, KUHARISHA YAIKUMBA MSUMBIJI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
4/04/2019 09:13:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: