Loading...

CHADEMA YAWEKA BAYANA MSIMAMO WAKE USHIRIKIANO NA ACT - WAZALENDO UCHAGUZI MKUU 2020

Loading...
Mkoani Kigoma. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakijafanya makubaliano yoyote na Chama cha ACT- Wazalendo kuachiana majimbo katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.

Hayo yalisemwa jana Ijumaa Mei 3 na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa matawi na kata wa chama hicho kutoka majimbo ya Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini.

Aliwataka wanachama na viongozi wa chama hicho kujenga chama ili kipate ushindi katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.

"Kuna mambo tulishirikiana na ACT-Wazalendo na vyama vingine vya upinzani hasa kwenye mchakato wa muswada wa vyama vya siasa ambao kimsingi wote tulikuwa na hoja inayofanana, kupinga muswada."

"Ndani ya Bunge tunashirikiana na Zitto (Kabwe-Mbunge wa Kigoma Mjini-ACT-Wazalendo) na chama chake, lakini nje ya Bunge hatuna ushirikiano wowote," alisema.

Mwalimu amesema endapo vyama hivyo vitakubaliana kushirikiana watatazama chama kipi kina nguvu eneo gani ili kuondoa migogoro iliyotokea mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu.

"Hatutakubali kugawana majimbo mezani kama tulivyofanya mwaka 2015 ambapo mojawapo ya mifano mibaya ni mgogoro uliotokea jimbo la Buhigwe kwa Ukawa kusimamisha wagombea wawili na CCM ikapata ushindi," alisema Mwalimu.
Na Aziza Omari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
CHADEMA YAWEKA BAYANA MSIMAMO WAKE USHIRIKIANO NA ACT - WAZALENDO UCHAGUZI MKUU 2020 CHADEMA YAWEKA BAYANA MSIMAMO WAKE USHIRIKIANO NA ACT - WAZALENDO UCHAGUZI MKUU 2020 Reviewed by By News Reporter on 5/04/2019 09:14:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.