Loading...

UJERUMANI TAYARI KUIPOKEA RAMADHANI, WAISLAM ELFU 40 KUPATA IFTARI BURE

Loading...
Ushirika wa kiislamu wa kituruki unaoshughulikia masuala ya dini (DITIB) wenye makao yake makuu mjini Kolon nchini Ujerumani, utafuturisha watu zaidi ya elfu 40 kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani katika msikiti wake mkuu wa mjini Kolon.

Kiongozi mkuu wa DITIB Kazım Türkmen, amesema sio Kolon peke yake bali katika misikiti yao 857 nchini Ujerumani kutakuwa na shughuli mbalimbali kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani.

Türkmen, alikumbushia kwamba siku ya jumapili wataswali swal aya kwanza ya Taraweh na jumatatu ndio mfungo wa Ramadhani utaanza rasmi nchini Ujerumani, aliongeza kwamba DITIB itafutarisha katika moja ya tatu ya misikiti yake 857 nchini humo.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UJERUMANI TAYARI KUIPOKEA RAMADHANI, WAISLAM ELFU 40 KUPATA IFTARI BURE UJERUMANI TAYARI KUIPOKEA RAMADHANI, WAISLAM ELFU 40 KUPATA IFTARI BURE Reviewed by By News Reporter on 5/04/2019 09:31:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.