Loading...

RAIS MAGUFULI ANATAKA MAMBO YAFANYIKE KISHERIA: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Loading...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amesema, Serikali inatambua mchango wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika ( TLS) katika  kuimarisha na kudumisha Utawala wa Sheria nchini.

Akasema  wakati wote  Serikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri kutoka TLS ilimradi kwamba,  maoni au ushauri huo unajikita katika kujenga, kuimarisha, hauegemei upande wowote, wenye staha na  usio na mashinikizo.

“ Kwanza niwashukuru sana kwa kuja kukutana  na kufanya mazungumzo nami, niwapongeze wewe Rais kwa kuchaguliwa  kuwa Rais wa TLS pamoja na wote mliochaguliwa katika baraza la uongozi.  Ni matumaini yangu kwamba, hamtawaangusha wanachama wenu waliowachagua, msiwaagushe tafadhali”  Akasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuongeza

“Wakati wote Serikali  imekuwa ikithamini sana mchango wenu na maoni yenu. Na kwa kweli mmekuwa mkitoa mchango  na maoni mazuri sana, niwahakikishe kwamba Serikali wakati wote ipo tayari kushirikiana nanyi. Jambo la muhimu ni  kuwa na majadiliano ( dialogue) pale ambapo  mnaona kunajambo la kujadiliana kabla ya  kulitolea matamko,” amesema.

Ameendelea kwa kusema, “Niwahakikishe kwamba, Serikali kwa ujumla na hasa Mhe. Rais John Pombe Magufuli  katika uongozi wake anapenda sana Sheria na anataka mambo yafanyike kisheria na kwa kuzingatia sheria ” akasisitiza Profesa Kilangi

Mazungumzo  kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na  Ujumbe wa Balaza la Uongozi yaliyochukua zaidi ya  masaa matatu, yalifanyika siku ya Alhamisi katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mitumba- Ihumwa  Jijini Dodoma.
Na Fatma Pembe.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI ANATAKA MAMBO YAFANYIKE KISHERIA: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI RAIS MAGUFULI ANATAKA MAMBO YAFANYIKE KISHERIA: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI Reviewed by By News Reporter on 5/04/2019 09:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.