Loading...

TAHADHARI JUU YA TAARIFA YA MIFUKO YA PLASTIKI INAYOSAMBAA

Loading...
Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuwataarifu wananchi kuwa taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii inayosema: "MIFUKO YA PLASTIKI KUENDELEA KUTIMIKA KWA SASA" si sahihi.

Katazo la Matumizi ya mifuko ya plastiki linabaki kuwa tarehe 01 Juni 2019 kama ilivyotangazwa na Serikali hapo awali. Ikumbukwe kuwa adhabu kwa wazalishaji, wauzaji na watumiaji wa mifuko ya plastiki inayopigwa marufuku zitatolewa kwa wote watakaokaidi.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawaasa watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea wasiliana nasi kwa namba ya simu ifuatayo: 0685333444.
Na Sheila Bakari.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAHADHARI JUU YA TAARIFA YA MIFUKO YA PLASTIKI INAYOSAMBAA TAHADHARI JUU YA TAARIFA YA MIFUKO YA PLASTIKI INAYOSAMBAA Reviewed by By News Reporter on 5/11/2019 09:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.