Loading...

KIM NA KANYE WEST WAMKARIBISHA MTOTO MWINGINE

Loading...
Kim West ambaye ni Nyota wa kipindi cha Televisheni cha maisha halisi kinachofaamika kama The Keeping Up with the Kardashians , mwenye umri wa miaka 38, amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba yeye na mumewe Kanye West, mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka wamemkaribisha mtoto wao wa kiume wa nne kwa uzazi wa kusaidiwa.

"Yuko hapa na hana kasoro!" Kardashian West alituma ujumbe wa Tweeter.

Kim na Kanye walikuwa na watoto watatu akiwemo mvulana anayeitwa Saint na msichana anayeitwa North
Ilithibitishwa mwezi wa januari kwamba wawili hao wangempokea mtoto wa nne ambaye angejiunga na ndugu zake wakiwemo wasichana Chicago, mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu na North, atakayetimiza umri wa miaka 6 mwezi ujao pamoja na Saint, mwenye umri wa miaka 3.

Taarifa kwamba mtoto huyo wao ambaye angezaliwa kupitia mwanamke mwingine alikuwa katika chumba cha uzazi zilifahamika Alhamisi wiki hii wakati wa kipindi cha The Ellen DeGeneres Show.

Kardarshians Januari 14 , Kardashian West alithibitisha taarifa juu ya ujauzito wa mwanae kupitia mwanamke ambaye hakutajwa jina baada ya kuulizwa iwapo ''anampango wa kumpata mtoto mwingine''

"Ndio tunao," alijibu nyota huyo wa kipindi cha maisha halisi, na kuongeza kuwa mtoto anakaribia kuzaliwa "hivi karibuni ."

"Ni mvulana, Nadhani hili limekuwa likihfahamika ,"alisema Kardashian West. "nililewa wakati wa sherehe zetu za Christmas na nikawaambia baadhi ya watu. Siwezi kukumbukani nani nilimwambia kwasabababu kwa sijawahi kulewa." Kim hakuelezea ni lini hasa atazaliwa, licha ya kusema atazaliwa hivi karibuni

Awali Kim alisema kuwa kuongezeka kwa uhalifu wa bunduki nchini Marekani kulimfanya 'asite' kupata watoto zaidi wakati alipokuwa akifanya kipindi cha Keeping Up With The Kardashians mwaka 2018.

lakini pia akasema kuwa Kanye alikuwa anataka sana kupata watoto zaidi, akisema kuwa a;limwambia anataka watoto jumla saba.

Kim alionywa na madaktari kuwa asijaribu kupata mtoto mwingine kutokana na matatizo ya kiafya aliyo nayo.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIM NA KANYE WEST WAMKARIBISHA MTOTO MWINGINE KIM NA KANYE WEST WAMKARIBISHA MTOTO MWINGINE Reviewed by By News Reporter on 5/12/2019 06:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.