Loading...

WAZEE ZAIDI YA 1,300 WANEEMEKA KWA MATIBABU

Loading...
WAZEE 1358 wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, ambao wamefikisha umri wa miaka 60 na kuendelea, wamepatiwa vitambulisho vya matibabu, ikiwa ni hatua ya serikali katika kuhakikisha wananchi walio fikisha umri wa kuzeeka wanapata matibabu.

Pia kuhakikisha wanakuwa na afya njema katika kutoa mchango wa mawazo yao ya kimaendeleo katika maeneo wanayoishi.

Vitambulisho hivyo vilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, wakati wa hafla fupi katika Kata ya Mabatini, huku akionya vikali watu ambao hawakidhi vigezo, lakini wanajiingiza katika kundi la wazee kuwa watambue watakapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Serikali ya Rais John Magufuli, imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003, pamoja na maelekezo yaliyoainishwa kwenye sera ya afya ya mwaka 2007 yenye lengo la kuhakikisha wazee wa Tanzania wanatambulika, kupewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayo husu maisha yao,  hivyo tuwe waaminifu katika suala hili la matibabu bure," alisema Mongella.

Aidha Mongella, aliwakemea watemdaji walio katika hospitali, zahanati na vituo vya afya kuacha tabia ya kuwanyanyapaa wazee.

Akisoma taarifa ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Editha Ngowi, mratibu wa wazee na watu wenye ulemavu, alisema tangu mwaka 2012 jumla ya vitambulisho 9,126 vimeshagawiwa, na jumla ya wazee 10,193 sawa na asilimia 79 wamepata.

"Upatikanaji na utolewaji wa matibabu kwa wazee umekuwa na changamoto mbali mbali, ambazo halmashauri imekuwa ikizifanyia kazi kwa namna moja…upungufu wa dawa za wazee kwenye vituo vya kutolea huduma na ukosefu wa makazi ya kulelea wazee kwenye wilaya ya Nyamagana," alisema Ngowi.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAZEE ZAIDI YA 1,300 WANEEMEKA KWA MATIBABU WAZEE ZAIDI YA 1,300 WANEEMEKA KWA MATIBABU Reviewed by By News Reporter on 5/12/2019 06:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.