Loading...

GIGY MONEY KUVISHWA PETE NA MSANII MWENZAKE KUTOKA NIGERIA

Loading...
Msanii  wa bongo fleva Gift Stanford maarufu kama 'Gigy Money' anayetamba na wimbo wake wa chanyanga,  amesema kuwa hivi karibuni kwenye siku yake ya kuzaliwa atavalishwa pete ya uchumba na mchumba wake mpya ambae pia ni mwanamziki mwenzake kutoka Nigeria.

Amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Refresh na Wasafi Tv wakati akieleza mipango yake ya mbeleni na mchumba wake ambaye anaishi naye kwa sasa na tayari wamesha shirikiana kwenye kazi ya muziki

Ameongeza kuwa mbali na mapenzi kwa sasa anaangalia sana kufanya kazi ambapo anajiandaa kutoa albamu ya nyimbo zake.

Aidha amesema wanenguaji (video vixin) wengi wamekuwa wanaingia kwenye muziki kutokana na ushawishi wanaoupata kutokana na wasanii wanaofanya nao kazi, ameongeza mbali na kazi yeye ni mama na anafanya muziki kwa malengo.
Na Mussa Chachala.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
GIGY MONEY KUVISHWA PETE NA MSANII MWENZAKE KUTOKA NIGERIA GIGY MONEY KUVISHWA PETE NA MSANII MWENZAKE KUTOKA NIGERIA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 5/05/2019 09:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.