Loading...

KIMBUNGA FANI CHATIKISA INDIA, IDADI YA VIFO YAONGEZEKA

Loading...
Idadi ya wale waliokufa katika Kimbunga Fani,kilichopiga ukanda wa pwani mashariki mwa India mwanzoni mwa mwezi huu imefikia 64.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, viongozi wa kituo cha operesheni ya dharura walitangaza kuwa baada ya miaka 43, idadi ya watu waliopoteza maisha yao iliongezeka hadi 64 kutokana na msimu wa kwanza wa majira ya kimbunga Fani, kilichopiga Ghuba ya Bengal.

Katika Kimbunga hicho, watu 241 wameripotiwa kujeruhiwa.

Barabara,umeme na mawasiliano ni kati ya  vitu vilivyoharibiwa kwa kiasi kikubwa na kimbunga hicho.

Mamilioni ya watu wamehamishwa makazi yao kabla ya kutokea kwa kimbunga.
Na Saidi Juma.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIMBUNGA FANI CHATIKISA INDIA, IDADI YA VIFO YAONGEZEKA KIMBUNGA FANI CHATIKISA INDIA, IDADI YA VIFO YAONGEZEKA Reviewed by By News Reporter on 5/14/2019 07:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.