Loading...

VITA YA KIBIASHARA KATI YA CHINA NA MAREKANI YAPAMBA MOTO, CHINA AJIBU MAPIGO

Loading...
China imesema leo kuwa itaongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani za thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi, katika hatua ya kujibu duru ya karibuni ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China na mipango ya Marekani kuzilenga bidhaa zote zinazoingizwa nchini mwake kutoka China. 

Tangazo hilo limekuja baada ya mazungumzo ya karibuni kabisa ya biashara kati ya Marekani na China kumalizika Ijumaa bila makubaliano, na baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 200. 

Licha ya hatua hiyo ya kulipiza kisasi, China imeonekana kutoa muda zaidi wa hadi Juni mosi. Ushuru mpya utazilenga bidhaa kadhaa za Marekani kuanzia asilimia tano hadi 25. 

Jibu la China limetangazwa mara tu baada ya Trump kuionya kutolipiza kisasi. Awali, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Geng Shuang alisema kuwa China hitawahi kusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
VITA YA KIBIASHARA KATI YA CHINA NA MAREKANI YAPAMBA MOTO, CHINA AJIBU MAPIGO VITA YA KIBIASHARA KATI YA CHINA NA MAREKANI YAPAMBA MOTO, CHINA AJIBU MAPIGO Reviewed by By News Reporter on 5/14/2019 06:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.