Loading...

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Loading...
Waislamu Tanzania na ulimwenguni kote wanaendelea na mfungo wao wa mwezi mtukufu wa Ramadan ulioanza kuadhimishwa rasmi wiki iliyopita.

Kufunga wakati wa mwezi huu mtukufu ni mojawapo wa nguzo 5 za Kiislamu ambazo kila Muislamu ni lazima kuzitimiza katika maisha yake.

Katika mwezi huu Waislamu hufunga kati ya siku 30 ama 29 kulingana na kuandama kwa mwezi kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu.

Hapa ni mifano ya hali inayoweza kuharibu Swawm kwa anayefunga katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani;

1. Kula na kunywa kwa makusudi. 
Na sio kwa kusahau wala kwa bahati mbaya au kwa kulazimishwa, katika mchana wa Swawm. 

2. Kujitapisha kwa makusudi. 
Kujitapisha huko ni kule kwa kutia kidole mdomoni au kunusa kitu kitachopelekea kutapika. 

3. Mume kumwingilia mke wake ama kumkumbatia au kumchezea hadi yakamtoka manii wakati wa funga. 

4. Kupiga punyeto (hadi kutoa manii) kwa makusudi ama kwa kutumia mkono au kwa kuchezewa na mkeo au kwa njia yoyote ile. 
Lakini manii zikitoka kupitia ndoto au kutazama (bila kukusudia) basi haiwezi kuharibu Swawm. 

5. Kupatwa na hedhi kwa mwanamke. 
Na hii ni hata kukiwa kutokea huko kuwa ni wakati wa kukaribia kufuturu/kufutari. 

6. Mwenye kutia nia ya kula wakati amefunga, kwa sharti kuwa kaazimia tendo hilo hata kama hakulitekeleza. 

7. Kudhania kuwa jua lishazama Magharibi au bado hakujapambazuka (yaani haujaanza wakati wa kufunga), kisha anayefunga akala, akanywa au akamuingilia mke wake.
Na Baraka Yusuf.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI Reviewed by By News Reporter on 5/17/2019 10:23:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.