Loading...

FAHAMU KUHUSU KICHAA CHA MBWA

Loading...
Kichaa cha mbwa ni nini? Inaelezwa kuwa ugonjwa hatari unaoathiri ubongo na kwa kawaida usipowahiwa kimatibabu, aliyeambukizwa anapoteza maisha.

Ikirejewa tena, cha kujuuliza, chanzo chake nini? Hilo niambukizo la virusi vinavyosababisha uvimbe wa ubongo, vinavyomtokea binadamu, mnyama au ndege.

Lakini, ni mara chache kuwapata wanyamawala majanina maambukizo kutoka mtu mgonjwa kwenda mwingine, ni mara chache sana.

Asilimia99 ya watu huambukizwa na mbwa. Pia, maradhi hayo yanayowatokea wanyama kama vilepaka,mbwehanambwa mwitu.

Maambukizo ya maradhi hayo hupitiamatenadamu, hasa kwa kung'atwa na mnyama anayeumwa. Ni mate kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa yanayoweza kusambaza kichaa cha mbwa, hasa yanapokutana na utando telezi wa mnyama mwingine au binadamu.

DALILI ZAKE

Ugonjwa hugundulika, baada ya dalili  kuonekana, ikijumuishwa na homa kali. Hilo linafuatwa na dalili kama:Kukasirika au kuogopa ghafla; kuyaogopa maji; kukosa uwezo wa kutawala mwendo waviungovya mwili; nakupoteza fahamu.

Inaelezwa, mara dalili hizo zinapoonekana, maana yake ugonjwa umeshaanza kuharibu ubongo na mishipa midogo, hatua ya mwisho ikiwa ni kifo cha mgonjwa.

Muda kati ya kuambukizwa ugonjwa na mwanzo wa dalili, kawaida huchukua wastani wamwezimmoja hadi mitatu.

Hata hivyo, kipindi hicho kinaweza kutofautiana, ikazidi kufikia mwaka au kwa wiki kadhaa chini ya mwezi mmoja.

Sababu kuu ni namna virusi lazima kusafiri vinavyosafiri kufikiamfumo mkuu wa ‘neva.’

TIBA NA KINGA

Watu wanaotibiwa mara moja baada ya kuambukizwa wanaweza kupona. Lakini,tibainahitaji kutekelezwa kabla ya virusi havijaifikia ubongo.

Ni kawaida katika nchi nyingi, wanyama wengi hupewachanjoza kujikinga ili wawe salama dhidi ya ugonjwa huo.

Kudhibiti wanyama na mipango ya chanjo zinapunguza hatari ya kichaa cha mbwa katika nchi kadhaa na kuchanja watu, kulipendekezwa kwa walio na hatari kubwa.

Kina nani wako hatarini? Hapo kunatajwa kundi la wanaofanya kazi na watumia muda mrefu katika maeneo ambayo kichaa mbwa ni kawaida.

Inashauriwa kuosha mahali panapoumwa na mchukubo kwa dakika 15, kwa kutumiasabunina nyenzo nyingime za usafi kuua virusi vya kichaa cha mbwa.

Inaelezwa, asilimia 95 ya vifo hivyo hutokea katika BaraAsianaAfrika. Hadi sasa inaelezwa maradhi hayo yako katika nchi zaidi ya 150 duniani.
Na Timoth Anthony.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FAHAMU KUHUSU KICHAA CHA MBWA FAHAMU KUHUSU KICHAA CHA MBWA Reviewed by By News Reporter on 5/17/2019 07:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.