Loading...

WANAUME WA KIAFRIKA HAWAJUI MAPENZI - MCHUNGAJI OBENG

Loading...
Mkuu na mwanzilishi wa Kanisa la Calvary Charistmatic Centre, Mchungaji Ransford Obeng wa Ghana amewasuta wanaume wa Afrika na kusema ni wabinafsi na wasiojua kupenda. 

Obeng anadai kuwa mwanaume ambaye anamtumia mkewe kama mtumwa bila ya kumjali basi hajui maana ya mapenzi.

Mchungaji huyo, alitoa matamshi hayo akihubiri kwenye kanisa lake ilivyoripotiwa katika YEN.com "Hapa Afrika, utampata mwanamke na mumewe wakitoka shambani, mke huwa amebebeshwa mizigo mingi bila kusahau mtoto huku mumewe akifuata akiwa na jembe.

Kisha mama huyo anapaswa kufika nyumbani ampikie mumewe chakula akiwa amejistarehesha kwenye kivuli," Obeng alisema. 

Alifafanua zaidi na kusema kuwa, baada ya mke kutayarisha chakula na kupeleka mezani, sehemu nzuri ya chakula hicho hupewa mume. 

"Afrika, chakula kikipikwa mwanamume anapewa sehemu nzuri. Mwanamke anapaswa kumchotea mumewe maji ya kuoga na kisha kurejea jikoni kuosha vyombo. Akimaliza mumewe atakuwa amejailaza kitandani na nguvu mpya" alidokeza Obeng.

Hata hivyo, ujumbe wake huenda ukaibua hisia mseto kwani wanaume wa kiafrika huwa wamewatwika wanawake na majukumu ya nyumbani.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAUME WA KIAFRIKA HAWAJUI MAPENZI - MCHUNGAJI OBENG WANAUME WA KIAFRIKA HAWAJUI MAPENZI - MCHUNGAJI OBENG Reviewed by By News Reporter on 5/27/2019 07:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.