Loading...

JAMBAZI AZIIBIA BENKI MAMILIONI AKITUMIA 'PARACHICHI' KAMA SILAHA

Loading...
Jambazi mmoja wa nchini Israeli aliwalaghai waathiriwa wake akili huku akiziibia benki mbili akitumia parachichi. 

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 47 alianza ujambazi wake katika benki ya Beersheba

Kulingana na gazeti la Times of Israel, jambazi huyo alitoa parachichi nyeusi na akawatishia kuwa ilikuwa ni bomu na atawalipua iwapo hawatampa fedha hizo. 

Alipokea kitita chake na akaondoka huku akitabasamu kimoyomoyo. 

Siku tano baadaye, alirudi kwenye benki tofauti na kufanya vivyo hivyo.

Kwenye benki hiyo alifanikiwa kuiba shilingi milioni 7.4, kabla ya maafisa wa polisi kumsaka na kumtia mbaroni. 

Maafisa wa polisi walishangaa kugundua kuwa silaha aliyokuwa akitumia kutishia wafanyakazi wa benki ilikuwa ni parachichi iliyokuwa imepakwa rangi ili ionekane kama kilipuzi.

Wafanyikazi wa benki waliwachwa kinywa wazi baada ya kujua waliibiwa na 'parachichi'!
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMBAZI AZIIBIA BENKI MAMILIONI AKITUMIA 'PARACHICHI' KAMA SILAHA JAMBAZI AZIIBIA BENKI MAMILIONI AKITUMIA 'PARACHICHI' KAMA SILAHA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 6/12/2019 08:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.