Loading...
Boris Johnson ameibuka na ushindi wa kura 126 kati ya kura 313 katika duru hii ya pili ya uchaguzi iliyofanyika Jumanne, ambayo inahusisha wagombea sita wenye kuwania nafasi ya kumrithi waziri Theresa May kwa nafasi ya uongozi wa chama.
Aliyemfuatia katika mchuano huo alikuwa waziri wa mashauri ya kigeni wa sasa Jeremxy Hunt aliepata kura 46 tu.
Hunt anakwenda katika duru ya inayofuata ya uchaguzi akiwa sambamba waziri wa mazingira Michael Gove,waziri wa mambo ya ndani Sajid Javid na Rory Stewart.
Katika duru hiyo aliyekuwa waziri wa mpango wa Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya Brexit Dominic Raab aliondolewa.
Jumapili iliyopita mwamba wa kushinikiza Brexit, alionekana madhubuti katika mdahalo wa televisheni mbele ya wagombea wenziwe wanne katika mjadala huo.
Chaguzi zaidi zitaendelea juma hili, mpaka wapatikane wagombea wawili.Baadae wanachama wa 160,000 wanatarajiwa kuwapigia wagombea hao kuchagua mshindi, na matokoe yake kutarajiwa kutolewa katika juma linaloanza tarehe 22 mwezi ujao.
Maafisa wengi walijiuzulu Juni 7 baada ya kuishindwa kupata ridhaa ya bunge kwa Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya. Chanzo DPAE

Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MRITHI WA 'THERESA MAY' WAZIRI MKUU WA UINGEREZA HUYU HAPA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
6/20/2019 06:56:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: