Loading...

MAJI YAGUNDULIWA SAYARI YA MARS, 'MATUMAINI YA KUWEPO KWA UHAI YAZIDI KUPATIKANA'

Loading...
Watafiti wamepata ushahidi wa kwanza wa maji katika sayari ya Mars

Kile wanachoamini kuwa ziwa kiko katika eneo lenye barafu nyingi la kusini na lina ukubwa wa kilomita 20.

Utafiti wa awali ulipata ishara za maji yanayopita katika sakafu ya sayari hiyo, lakini hiyo ni ishara ya kwanza ya maji kuonekana katika sayari hiyo katika siku za hivi karibuni.

Maziwa yaliogunduliwa na Nasa yalionyesha kwamba maji yalikuwepo katika sakafu ya sayari hiyo katika siku za nyuma.

Hatahivyo, hali ya anga ya sayari hiyo ni baridi na hivyo basi kufanya maji yake kubadilika na kuganda.

Matokeo yake yanafurahisha kwa sababu wanasayansi wametafuta kwa muda mrefu ishara ya kuwepo kwa maji katika sayari ya Mars lakini hawakufanikiwa kupata ushahidi wowote.

Pia itawafurahisha wale wanaofanya utafiti wa kuwepo kwa uhai mbali na duniani-licha ya kwamba matokeo hayo hayajatoa ushahidi wowote wa kuwepo kwa viumbe.

Ugunduzi huo ulifanyika kwa kutumia kifaa chenye radar kilichokuwa ndani ya kituo cha anga cha Ulaya kwa jina Mars Express orbiter.

"Pengine huenda sio ziwa kubwa sana , alisema Profesa Orosei kutoka taasisi ya maswala ya angani inayohusika na asili ya nyota na viumbe vyengine vilivyopo mbinguni', alimbaye ndiye aliyeongoza utafiti huo.

Kifaa cha Marsis hakikuweza kubaini upana wa maji hayo, lakini kundi hilo la watafiti linakadiria kuwa na upana usiopungua mita moja.

''Hii ina inathibitisha kuwepo kwa ziwa lenye maji , na sio maji yalioyeyuka yaliopo kati ya mwamba na barafu, kama ilivyo katika maeneo mengine ya barafu duniani'', aliongeza Profesa Orosei.

Vifaa vyenye radar kama vile Marsis huchunguza sakafu ya sayari kwa kutuma mawimbi ya ishara na kuchunguza kile kitakachorudi.

Mstari mweupe uliopo juu ya picha unaonyesha mwanzo wa mkusanyiko wa maji yalioganda na kuwa barafu na vumbi.

Chini ya hilo, watafiti waligundua kitu kisicho cha kawaida yapata kilomita 1.5 chini ya barafu.

''Katika rangi ya samawati unaweza kuona kutoka chini ikilinganishwa na kutoka kwa sakafu. Hiki ni kitu kinachoonyesha wazi kwamba kuna ishara ya kuwepo kwa maji'' , alisema Profesa Orosei.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAJI YAGUNDULIWA SAYARI YA MARS, 'MATUMAINI YA KUWEPO KWA UHAI YAZIDI KUPATIKANA' MAJI YAGUNDULIWA SAYARI YA MARS, 'MATUMAINI YA KUWEPO KWA UHAI YAZIDI KUPATIKANA' Reviewed by GEOFREY MASHEL on 7/10/2019 05:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.