Loading...

BINTI WA MIAKA 11 ALIYEPEWA MIMBA NA KAKA YAKE AJIFUNGUA

Loading...
Binti wa miaka 11 amejifungua kichanga katika hospitali moja huko nchini Hispania baada ya kupewa ujauzito na kaka yake wa miaka 14.

Mama wa kichanga huyo alipewa ujauzito na kaka yake aliyekuwa na miaka 13. Binti huyo ambaye ni mkazi wa Bolivia kwa asili, hakuweza kujua kama ana ujauzito na familia yake kiujumla. Alifikishwa hospitalini akiwa na 'maumivu ya tumbo' lakini ikataarifiwa anakaribia kujifungua baada ya vipimo kufanywa na madaktari.

Binti huyo wa miaka 11 alijifungua katika hospitali ya Virgen de la Arrixaca mjini Murcia, Kusini Mashariki mwa nchi ya Hispania siku ya Ijumaa, Februari 2, 2018.

Maafisa polisi walitaarifiwa kwa ajili ya uchunguzi na baadae waligundua baba wa mtoto huyo alikuwa ni kaka yake ambaye mama yake ni raia wa Bolivia.

Mama na kichanga inasemekana wanaendelea vizuri. Mara tu baada ya kujifungua uongozi hospitalini hapo walipiga simu polisi na kwa ustawi wa jamii ili kufanya uchunguzi nani aliyempatia mimba hiyo.

Chanzo cha karibu na kesi hiyo kinasema kaka yake alikuwa na miaka 13 wakati dada yake aliposhika ujauzito na hakuna sheria yeyote ya Hispania itakayoweza kumshtaki kutokana na umri wake kuwa mdogo. "Kutokana na rika la mtuhumiwa na mama wa kichanga kuwa sawa hakuna kesi itakayofunguliwa labda uchunguzi uwe tofauti." alisema afisa mmoja wa polisi akiongea chombo cha habari nchini humo.
BINTI WA MIAKA 11 ALIYEPEWA MIMBA NA KAKA YAKE AJIFUNGUA BINTI WA MIAKA 11 ALIYEPEWA MIMBA NA KAKA YAKE AJIFUNGUA Reviewed by By News Reporter on 2/13/2018 10:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.