Loading...
MGUNDUZI wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma jana alilala milionea baada ya kuzawadiwa kitita cha Sh. milioni 100 na Rais John Magufuli kwa ugunduzi wake huo, bila kutarajia.
Rais Magufuli alitangaza kumpa mzee huyo fedha hizo jana kwenye mji mdogo wa Mirerani uliopo mkoani Manyara wakati akizindua ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite, uliojengwa na kikosi cha Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Rais Magufuli alisema jana kuwa alitumiwa ujumbe kwenye simu yake na mtu ambaye hakumtambua kuhusu shida anazopata mgunduzi huyo ambaye kwa sasa ni mgonjwa wa kiharusi, ikiwemo kutotambuliwa ugunduzi wake kwa miaka mingi.
Rais Magufuli aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwatambua watu wanaogundua vitu kama alivyofanya mzee Ngoma kwenye madini hayo.
Alisema Ngoma aligundua madini hayo mwaka 1967 akiwa katika kijiji cha Mirerani na akasema hivyo ni vizuri Watanzania wakajua kuwa aliyegundua madini hayo ni Mtanzania mwenzetu na wala siyo mtu kutoka nje ya nchi.
“Niliambiwa huyo mzee amepooza na niliambiwa na mtu kwa kutumiwa meseji, na huyo mzee amehangaika toka mwaka 1967 mpaka leo; na leo niliagiza aletwe mpaka hapa ili Watanzania wamuone mtu ambaye anawanufaisha watu wengi," alisema Rais Magufuli.
“Serikali yangu itampatia Sh. milioni 100 kwa ajili ya kupata matibabu ya mguu uliopooza na kwa ajili ya matumizi mengine mbalimbali halafu baadaye itaona nanma ya kuendelea kuuthamini mchango wake mpaka hapo Mungu atakapoamua,” alisema Rais Magufuli na kushangiliwa na umati wa wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
“Hapa (nchini) hata ufanye chochote hata kama ni kizuri namna gani, hata ungegundua nini, ninafahamu wagunduzi wengi Chuo Kikuu lakini hawakutambuliwa.
"Hata mimi niligundua kitu fulani cha kemia lakini nilivyoomba kutambuliwa mpaka leo wamebaki na kitabu changu kwenye Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.”
Alionyesha kusikitishwa sana na Watanzania ambao wamekuwa hawathamini mchango wa watu wanaogundua vitu, huku akimtaja mzee Ngoma kugundua madini hayo na kupeleka barua kwa Mjiolojia Septemba 23, 1967 ili kumuonesha alivyogundua ili na yeye aweze kutambuliwa.
Wakati wa hafla hiyo jana, Rais Magufuli aliwaagiza watendaji wake wampeleke mzee huyo akakae jukwaa kuu ili atambuliwe kama mgunduzi wa madini ya Tanzanite.
Rais Magufuli alitoa wito kwa Watanzania kuwathamini watu wanaofanya vizuri katika nchi.
“Wapo watu wanaotajirika, wapo waliokuwa mabilionea na sio Watanzania kwa sababu dhahabu inasombwa kwenda nje, huyu amebaki hivyo hivyo, Mungu atusaidie ile mioyo ya fitina iwe inaondoka ili tuwatambue wenzetu,” alisisitiza.
Rais Magufuli alisema alipata habari kwa kuandikiwa ujumbe mfupi na baadaye kupata taarifa kupitia mtoto wake, Hassan Ngoma na walipochunguza walibaini ukweli kuhusu mzee huyo.
“Huu ni mwanzo mzuri wa kuwakumbuka watu wa namna hii, madini haya yalikuwa yanasombwa na kama ni kuisha ungekuta yameisha.”
Alipopewa nafasi ya kuzungumza chochote na Magufuli baada ya hotuba yake, Ngoma alisema anawahakikishia Watanzania kuwa wamempata Rais wa wanyonge na akasema amechaguliwa na Mungu.
Asha Ngoma, mtoto mwingine wa mzee huyo alisema yeye ndiye alimtumia ujumbe mfupi Rais, na kwamba hakuamini kama angemjibu na akadai jina la madini hayo awali yaliitwa Ziocite, ndipo baadayeyaliunganishwa Tanzania na Ziocite ikapatikana Tanzanite.
Ukuta wa Mirerani ambao umejengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 5.6 una urefu wa kilomita 24.5 na umevunja rekodi kwa kujengwa kwa muda mfupi kwa miezi mitatu badala ya sita kama ilivyopangwa.
Ulianza kujengwa mwezi Novemba mwaka 2017 na kukamilika mwezi Februari mwaka huu.
Rais Magufuli alimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, kwa kujenga ukuta huo kwa miezi mitatu badala ya sita iliyopangwa awali.
Na Geofrey Okechi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.

MGUNDUZI WA TANZANITE ALAMBA KITITA CHA MILIONI 100
Reviewed by By News Reporter
on
4/07/2018 07:01:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: