Loading...
Wasichana na wanawake hutumia vidonge vya kupanga uzazi kipindi ambapo wameshiriki ngono bila kinga na wakihofia kuwa wanaweza kupata uja uzito ambao hawakupanga.
Wengi hutumia tembe za Postinor-2 wanazozinunua kutoka kwenye maduka ya madawa huku baadhi yao wakitumia tembe za mwezi mzima za kupanga uzazi.
Kuna wale ambao hujikuta wameshiriki ngono na watu wasiowajua baada ya kunywa pombe usiku kucha na kurusha roho, hivyo hulazimika angalau kuzuia kupata uja uzito.
Hata hivyo, kuna madhara ambayo hutokana na matumizi ya dawa hizo ambazo wengi hawayajui:
1. Kupata hedhi za mara kwa mara, hasa katikati ya mzunguko
2. Uchungu kwenye matiti
3. Maumivu ya kichwa na kipandauso
4. Kuongezeka uzito
5. Mabadiliko ya hisia
6. Kukosa hedhi kwa kipindi
7. Kupungua kwa hamasa wakati wa ngono
8. Majimaji yanayotokea kwenye sehemu za uzazi
9. Kushindwa kuona vizuri kwa wale wanaotumia miwani za macho
10. Kuwa na vilia au vidonge vya damu
11. Maumivu ya tumbo na kiuno
12. Kujaa kwa miguu na mapaja na kusikia uchungu sehemu hizo
Na Peter Godwin.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MADHARA 14 USIYOYAJUA YA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO
Reviewed by By News Reporter
on
9/06/2018 03:21:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: