Loading...

RAIA WA CHINA ALIYEWAITA WAKENYA NYANI, MASIKINI NA WAPUMBAVU ATIWA MBARONI

Loading...
Raia wa China aliyenaswa katika video akisema Wakenya ni maskini, weusi na tumbili wachafu ametiwa mbaroni na anasubiri kufukuzwa nchini humo kwenda kwao. 

Liu Jiagi alikamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi, Septemba 6 baada ya video hiyo kusambaa kwa kasi mtandaoni na kuwaudhi Wakenya.

Jiagi ni mfanyakazi katika kampuni ya Sonlink (K) inayouza vifaa vya pikipiki mjini Ruiru, na matusi yake yaliwakera wengi waliotaka akamatwe na kisha afukuzwe humo nchini kwa tabia yake ya kibaguzi na kukosa adabu.

Wakenya wengi akiwamo Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na hata kiongozi wa Third Way Alliance Ekuru Aukot walitaka kufahamu aliko Mchina huyo ambaye alimkosea Rais Uhuru Kenyatta heshima.

Kukamatwa kwa Jiagi kulifanikiwa kupitia juhudi za Polisi na Idara ya Uhamiaji na kulingana na ripoti, kufikia usiku wa Jumatano, Septemba 5 alikuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JKIA wakimsubirisha ndege ya kumpeleka China.

Kwa muda sasa serikali imekuwa ikifanya uchunguzi kuhusiana na raia wa kigeni wanaoishi humu nchini bila ya vibali na idadi kubwa yao wamefukuzwa na kurejeshwa makwao.
Na Hamidu Bakari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIA WA CHINA ALIYEWAITA WAKENYA NYANI, MASIKINI NA WAPUMBAVU ATIWA MBARONI RAIA WA CHINA ALIYEWAITA WAKENYA NYANI, MASIKINI NA WAPUMBAVU ATIWA MBARONI Reviewed by By News Reporter on 9/06/2018 03:45:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.