Loading...

MGOMBEA WA URAIS BRAZIL MWENYE USHAWISHI MKUBWA ACHOMWA KISU

Loading...
Mgombea anayeongoza kuwa na ushawishi mkubwa anaweza kushinda uchaguzi nchini Brazili Jair Bolsonaro, amechomwa kisu wakati wa kampeni zake , mgombea huyo wa mrengo wa kulia alichomwa kisu katika mkutano mkubwa wenye mkusanyiko wa watu wengi katika eneo la kusini mashariki.

Mwanasiasa huyo ambaye amekua gumzo kwa maoni yake juu ya ubaguzi wa rangi , amepata kura nyingi katika kura za maoni za hivi karibuni.

Kura hizo za maoni zinaonesha kuwa anatafanya vizuri katika uchaguzi wa urais mwezi ujao na kumpita Mgombea na Rais wa zamani Lula da Silva.

Picha za video zimemuonesha bwana Bolsonaro akinyoosha mkono kwa wafuasi wake na hapo ndipo alipochomwa na kitu ambacho baadae iligundulika na kisu

Baada ya hapo aliinama kwa maumivu na haraka wafuasi wake walimshusha chini na kumuingiza ndani ya Gari kisha kupelekwa Hospitali.
Na Marry Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MGOMBEA WA URAIS BRAZIL MWENYE USHAWISHI MKUBWA ACHOMWA KISU MGOMBEA WA URAIS BRAZIL MWENYE USHAWISHI MKUBWA ACHOMWA KISU Reviewed by By News Reporter on 9/07/2018 05:10:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.