Loading...
Bunge la Ethiopia limemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwananmke wa nchi hiyo. Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo, kunafuatia kuteuliwa kwa baraza la mawaziri lenye idadi sawa ya wanaume na wanawake.
Sahle-Work Zewde ambaye ni mwanadiplomasia wa muda mrefu, anachukuwa nafasi ya Mulatu Teshome ambaye amejiuzulu wadhifa wa urais ambao nchini Ethiopia ni wa heshima tu. Baada ya kuchaguliwa kwake, Sahle-Work amesema kuingia madarakani kwa waziri mkuu Abiy Ahmed ni hatua ya mfano mwema, ambayo anaamini itasaidia kuleta amani nchini Ethiopia ambako mnamo miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mizozo mingi yenye msingi wa kikabila.
Fitsum Arega ambaye ni kiongozi wa ofisi ya waziri mkuu Abiy Ahmed, amesema kupitia ukurasa wake wa twitter, kwamba kuchaguliwa kwa rais mwanamke katika nchi ya Ethiopia ambayo ni jamii ya mfumo dume, sio tu kutoa mfano wa kuigwa kwa mustakabali wa nchi, bali pia kunafanya ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi muhimu kuwa kitu cha kawaida.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

ETHIOPIA YAMPATA RAIS WA KWANZA MWANAMKE, YAANDIKA HISTORIA
Reviewed by By News Reporter
on
10/25/2018 04:20:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: