Loading...

MABOMU YALIYOTUMWA KWA CLINTON NA OBAMA YAZUA TAHARUKI

Loading...
Maafisa nchini Marekani wameanzisha uchunguzi kujua ni nani alihusika na mabomu yaliyotumwa kwa marais wa zamani Barack Obama na Bill Clinton, viongozi wengine wa ngazi ya juu wa chama cha Democrats na kituo cha televisheni cha CNN.

Wakosoaji wa Rais wa Marekani Donald Trump wanamshutumu kwa kuchochea chuki na ghasia siku chache kuelekea uchaguzi wa kati kati ya muhula unaotarajiwa tarehe 6 Novemba.

Akizungumzia kisa hicho cha mabomu kutumwa kwa viongozi na vyombo vya habari, Trump alitoa wito wa kuwepo umoja lakini muda mfupi baadaye alivishambulia vyombo vya habari kwa kile alichokitaja uhasama wake usiokoma. 

Mara kwa mara Trump amekuwa akiishutumu CNN kwa kueneza habari za uongo na kuukosoa vikali utawala wake. 

Mkuu wa polisi wa New York James O'Neil amekiambia kituo hicho cha CNN kuwa wale waliohusika na kitisho hicho cha mabomu watajulikana na kukamatwa hivi karibuni.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MABOMU YALIYOTUMWA KWA CLINTON NA OBAMA YAZUA TAHARUKI MABOMU YALIYOTUMWA KWA CLINTON NA OBAMA YAZUA TAHARUKI Reviewed by By News Reporter on 10/25/2018 05:17:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.