Loading...

KANYE WEST APONDWA NA RAPA WA UGANDA

Rapa Gnl Zamba kutokea Uganda amtolea povu rapper Kanye West ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda pamoja na familia yake kwaajili ya kukamilisha Album yake ya Yandhi na kumuita Kanye West mbinafsi.

Rapa huyo ameeleza kuwa watu wa Uganda wanahitaji maji na sio viatu aina ya Yeezy alivyovitoa Kanye West kwa Rais Museveni siku ya October 15,2018  alipotembelea Ikulu, Kupitia ukurasa wa twitter wa Gnl Zamba ameyaandika hayo.
Loading...
ly: Verdana, sans-serif;">
"Kanye sio rapa wala msanii wa muziki wa Hip Hop, sio mwerevu ni mbinafsi, anijifikiria yeye na kujitegemea mwenyewe, Uganda sasa hivi inatumika , hayo ni mawazo yangu juu ya Mayuda weusi, Watu wanahitaji maji na sio Yeezys" --- Rapper Gnl Zamba

October 16,2018 Kanye West alitembelea moja ya kituo cha watoto yatima nchini humo na kugawa viatu aina ya ‘Yeezy’ kwa watoto hao na kuelezwa kuwa thamani ya idadi ya viatu alivyovitoa Kanye vinafikia thamani ya zaidi Tsh. Millioni 500.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KANYE WEST APONDWA NA RAPA WA UGANDA KANYE WEST APONDWA NA RAPA WA UGANDA Reviewed by By News Reporter on 10/18/2018 06:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.