Loading...

KENYA YAPIGA MARUFUKU SAMAKI WA KICHINA

Wafanyabiashara wa samaki wanashusha pumzi baada ya marufuku ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi ya Kenya mahsusi China kutangazwa. Rais Uhuru Kenyatta ametangaza marufuku hiyo Jumatano (17.10.2018)

Tangazo hilo la kupiga marufuku uagizaji samaki kutokea nchi za kigeni limetolewa baada ya wafanyabiashara wa sekta hiyo kulalamika kuhusu ushindani mkubwa sokoni.

Loading...
erif;">Akiwa kwenye kikao cha kujadili masuala ya wafanyabiashara wadogo katika chuo kikuu cha biashara cha Strathmore, Rais Uhuru Kenyatta alisisitiza kuwa ipo haja ya kuwa na ujanja kwenye biashara.

Mwezi wa Juni mwaka huu wavuvi kutokea eneo la ziwa Naivasha walilalamika kuwa samaki wa kigeni wamejaa sokoni jambo linalowasakama koo wafanyabishara wa humu nchini.Itakumbukwa kuwa mwaka 2016 gavana wa zamani wa kaunti ya Kisumu Jack Ranguma aliirai serikali kuu kuweka marufuku kamili ya kuagiza samaki kutokea nchi ya China kwani hilo linakwamisha biashara.
Na Halima Ramadhani.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KENYA YAPIGA MARUFUKU SAMAKI WA KICHINA KENYA YAPIGA MARUFUKU SAMAKI WA KICHINA Reviewed by By News Reporter on 10/18/2018 07:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.