Loading...
Kamanda Sirro leo amezungumza na vyombo vya habari juu ya sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji aliyetekwa na watu wasiojulikana juma lililopita.
IGP Sirro amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi linapiga kazi usiku na mchana kuhakikisha ndugu yetu na Mtanzania mwenzetu anapatikana akiwa salama.
Akizungumza na waandishi wa habari alikuwa na haya ya kutaarifu:
"Gari lililomteka Mo Dewji lilipitia barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kwenda mpaka Kawe"
"Gari iliyotumika katika utekaji wa Mohammed Dewji ni aina ya Toyota Surf na iliingia nchini tarehe 1 Oktoba ikitokea nchi jirani"
"Sidhani kama tunahitaji watu wa kuja kutusaidia. Lazima tutunze heshima ya nchi"
"Tunakagua 'apartment' kwa 'apartment' na kama utaona gari tuliyoitaja toa taarifa."
"Na watu wenye kamera binafsi wakiweza wasaidie kutoa taarifa ikibidi"
"Hao wahalifu tukiwakamata watajua kuwa hii ni Tanzania. Mimi huwa nasema nitakugonga kwa mujibu wa Sheria."
"Mpaka sasa tunawashikilia watu 8 na hao tuna sababu za kuendelea kuwashikilia."
Alipoulizwa kama Mo bado yupo hai au la, alikuwa na haya ya kujibu: "Suala la Mo kuwa hai au kutakuwa hai Mimi sina majibu."
"Kusema nchi gani imehusika bado ni mapema sana bado tuko kwenye uchunguzi"
"Tupeane taarifa sahihi na sio majungu. Watu wanasema Mo yuko sehemu flani lakini unagundua si kweli"
"Watu watoe taarifa sahihi ili kuisaidia nchi yetu"
"Tukio la kutekwa Mo Dewji tumekamata silaha 2 na tumezifanyia uchunguzi"
"Pia tumelitambua gari linaloweza kuwa lilihusika katika utekaji"
"Tumefuatilia CCTV Camera. Gari lililotumika limetokea nchi jirani"
Amewasa wananchi kuwa watulivu kwani Jeshi la Polisi linafanya kazi yake.
Na Peter Leornard.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MSAKO WA MO WAFIKIA PAZURI
Reviewed by By News Reporter
on
10/19/2018 01:37:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: