Loading...

ROSE MUHANDO KUREJEA UISLAMU

Loading...
Nyota Rose Muhando ametangaza kurudi tena katika dini yake ya kiislamu baada ya kusema kuwa amegundua kuwa ule upendo aliowahi kuambiwa upo katika ukristo hauoni zaidi ya majonzi na maumivu kila siku.

Habari za Rose Muhando zimekuwa zikisambaa sana hapa karibuni kutokana  kuwa mwanadada huyo kwa sasa amekuwa akionekana kama amechanganyikiwa sana na kuwa amefirisika na hata watoto wake hawana tena mahali pa kuishi.

"Wakati ninaokoka niliambiwa maneno ya upendo sana na kwamba nitakutana na upendo lakini badala yake nimekuwa nikikutana na matusi tu kila siku, kwa mfano mtu anakuhalika sehemu unashindwa kufika na unatoa taarifa lakini kesho yake unasikia kuwa anatangaza umemtapeli, wanashindwa kujua na kukumbuka hata jema moja kutoka kwangu. Nafikiria kurudi kwenye dini yangu ninaamini nitapata faraja."

Rose alikuwa moja ya wasanii wakubwa sana wa injili huku akisifiwa kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania kwa kazi zake, nyimbo zake zilikuwa zikipendwa na kila mtu bila kujali umri wala dini.
Na Ummy Kalisa.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ROSE MUHANDO KUREJEA UISLAMU ROSE MUHANDO KUREJEA UISLAMU Reviewed by By News Reporter on 11/24/2018 06:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.