Loading...
Baada ya nyota wa soka wa Brazil Ronaldinho, 38, kutangazwa kufilisika, masaibu yamemwandama, kwani maafisa wa polisi nchini humo walivamia jumba lake na kuchukua magari matatu ya kifahari.
Ronaldinho pamoja na kakake wanaandamwa na serikali nchini humo kuhusiana na madai kuwa taasisi yake ya kutoa msaada ilikuwa na deli la serikali kutokana faini ilizopigwa.
Kulingana na jarida la Sun la Uingereza, paspoti ya nyota huyo wa zamani wa Barcelona ilishikiliwa mwezi uliopita baada ya maafisa wa mashtaka wa serikali kugundua kuwa alisalia na Sh14,000 (sawa na paundi 5) pekee kwenye akaunti yake ya benki.
Wakati wa msako kwenye makazi yake, polisi walishikilia magari yake mawili aina ya BMW na gari lingine aina ya Mercedes kutokana na deni hilo la zaidi bilioni 4 (paundi 1.75 milioni).
Msako huo ulifanywa na kiongozi wa mashtaka ya haki na kulinda mazingira ya Brazil kwa nia ya kupata pesa hizo ambapo taasisi ya Ronaldinho ilipigwa faini.
Lakini Gaucho anaaminika kuwa na pesa lakini anasita kulipa faini za shirika lake.
Taasisi ya Ronaldinho Gaucho ilipigwa faini na wizara ya mazingira nchini Brazili kwa kuleta madhara ya kimazingira mwaka wa 2013.
Na Frank Zephania.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

POLISI WAMVAMIA RONALDINHO MDA MCHACHE BAADA YA KUTANGAZWA AMEFILISIKA
Reviewed by By News Reporter
on
11/24/2018 07:23:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: