Loading...

UCHAGUZI DRC: WAPINZANI WAUNGANA DRC, KUMUANGUSHA KABILA NA CHAMA CHAKE

Vyama viwili vikuu vya upinzani vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeungana baada ya kujiondoa kwenye muungano wa awali uliomuweka mgombea mmoja kushindana na yule anayeungwa mkono na Rais Joseph Kabila.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyotangazwa siku ya Ijumaa (23 Novemba) mjini Nairobi, Kenya, sasa Felix Tshisekedi anayeongoza chama kikubwa zaidi cha upinzani cha UPDS atasimama kwa niaba ya chama chake na kile cha spika wa zamani, Vital Kamerhe.

Uamuzi huu umefikiwa ikiwa ni mwezi mmoja tu kabla ya uchaguzi wa tarehe 23 Disemba kwenye taifa hi
Loading...
o tajiri kwa madini la Afrika ya Kati. 

Tangazo hili linamaanisha kwamba uchaguzi huu utakuwa na pande tatu kuu zinazowania: Emmanuel Ramazani Shadary anayeungwa mkono na Kabila, Martin Fayulu anayeungwa mkono na viongozi wawili wakuu wa upinzani waliozuiwa kuwania urais - Jean-Pierre Bemba na Moise Katumbi, na Tshisekedi anayeungwa mkono na Kamerhe.

Tshisekedi, mtoto wa kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, marehemu Etienne Tshisekedi, alitoa wito kwa wagombea wengine wa upinzani kumuunga mkono ili washinde uchaguzi huo.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UCHAGUZI DRC: WAPINZANI WAUNGANA DRC, KUMUANGUSHA KABILA NA CHAMA CHAKE UCHAGUZI DRC: WAPINZANI WAUNGANA DRC, KUMUANGUSHA KABILA NA CHAMA CHAKE Reviewed by By News Reporter on 11/27/2018 05:42:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.