Loading...

AJALI YA BOTI UGANDA: MIILI ZAIDI KUOKOLEWA, CHANZO CHA AJILI CHAJULIKANA

Shughuli ya kutafuta miili ya watu waliokuwa kwenye mashua iliyozama katika Ziwa Victoria nchini Uganda inaendelea, huku chanzo cha ajili hiyo kufichuliwa.

Taarifa za awali zinasema zaidi ya watu 90 walikuwa ndani ya mashua hiyo wakati iajali inatokea.

Maafisa wa uokoaji wamethibitisha kuwa maiti 33 zilikuwa zimeopolewa ziwani kufikia siku ya Jumapili jioni huku manusura 26 pia wakiokolewa.

Miongoni wa mwatu 26 walionusurika alikuwemo mwana wa Mfalume wa Buganda nduguye mfalme wa sasa wa Buganda, pamoja na wasanii mashuhuri wa Uganda.

Inadaiwa wasanii hao walikuwa wanajianda kuwatumbuiza watu kwenye boti hilo la burudani.
Loading...
br> ''Injini ya boti hiyo ilikuwa na hitilafu kwa sababu ilikuwa inazimika zimika, pia ilikuwa na tundu kubwa iliyokuwa ikiingiza maji ndani ya boti, na kuna wakati boti hiyo ilishindwa kuenda, '' alisema mmoja wa manusura wa boti hiyo.

Mashua hiyo iliyokuwa na watu waliokuwa wanaelekea sherehe, ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono.

Naibu waziri wa uchukuzi nchini Uganda Aggry Bagire anasema ''Boti hii ilikuwa halijasajiliwa wala kufanyiwa ukaguzi na timu yetu ilikuwa ikiitafuta kwa mda wa siku tatu''.

Wamiliki wake walijua kuwa iko katika hali mbaya kiufundi lakini wakalazimisha kufanya safari nayo.

Kisa hiki kimezusha mjadala miongoni mwa wananchi kuhusu usimamizi na usalama wa safari za majini nchini Uganda.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AJALI YA BOTI UGANDA: MIILI ZAIDI KUOKOLEWA, CHANZO CHA AJILI CHAJULIKANA AJALI YA BOTI UGANDA: MIILI ZAIDI KUOKOLEWA, CHANZO CHA AJILI CHAJULIKANA Reviewed by By News Reporter on 11/27/2018 05:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.