Loading...

BAA KUFUNGULIWA MASAA 24, MAKONDA AANDAA MPANGO

Loading...
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema anaandaa utaratibu ili wafanyabishara mbalimbali, wakiwamo wa baa waanze kufanya kazi kwa saa  24.

Wakati akitangaza neema hiyo, Makonda pia ameeleza kushangazwa na utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni wa kudai vyeti vya ndoa, unaowafanya wakose mapato.

Makonda aliyasema  hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya, makatibu tawala, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa mkoa huo, kuhusu mkakati wa kukusanya mapato bila kuwabughudhi wafanyabishara.

"Maana ya Jiji la Dar es Salaam kuwa Jiji la kibishara ni pamoja na kuwawezesha wafanyabishara kufanya kazi kwa saa 24. Kwa sasa baa zinafunguliwa hadi saa sita  usiku lakini mpango wetu zifunguliwe muda wote ili serikali ipate mapato," alisema Makonda.

Makonda alisema kwa sasa sheria iliyopo inaruhusu biashara za baa kufanyika hadi saa 8:00 usiku tofauti na awali ilikuwa mwisho saa 6:00 usiku lakini kuna baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakiwasumbua wafanyabishara kinyume cha taratibu zilizowekwa.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BAA KUFUNGULIWA MASAA 24, MAKONDA AANDAA MPANGO BAA KUFUNGULIWA MASAA 24, MAKONDA AANDAA MPANGO Reviewed by By News Reporter on 1/05/2019 10:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.