Loading...

HUYU NDIYO MRITHI WA DIAMOND KWA ZARI

Mke wa zamani wa Nyota Diamond Platinumz, Zari 'Boss Lady' Hassan pamoja na watoto wake watatu wa kiume walisherehekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya nchini Uganda.

Wakiwa Uganda, familia hiyo ilikutana na watu kadhaa wakiwemo marafiki wao wa zamani pamoja na ndugu na jamaa zao.

Mmoja wa walionekana wakijivinjari na Zari alikuwa William Bugeme kwa majina ya usanii Boss Mutoto, ambaye ni rafiki wa zamani wa marehemu muwewe wa zamani Zari, Ivan Ssemwanga.

Zari na Boss Mutoto wanadaiwa kutoka kimapenzi, na hii ni
Loading...
tangu Zari alipokuwa kwenye ndoa na mwanamuziki Diamond Platinumz.

Wawili hao walionekana wakila bata pamoja katika maeneo tofauti ya burudani kulingana na picha alizorusha kwenye mitandao ya kijamii Boss Mutoto.

Hata hivyo, Zari hajachapisha picha zozote akiwa na Boss Mutoto ila alionekena akiwa pekee yake na wanawe.

Aidha, wawili hao wamekana vikali madai kwamba ni wapenzi, walidai wao ni kaka na dada wanaofaana katika kila hali.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HUYU NDIYO MRITHI WA DIAMOND KWA ZARI HUYU NDIYO MRITHI WA DIAMOND KWA ZARI Reviewed by By News Reporter on 1/05/2019 09:53:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.