Loading...

FILAMU YA MWANAMUZIKI KUTOKA ZANZIBAR YAZOA TUZO

Loading...
Filamu ya Bohemian Rhapsody inayohusu maisha ya muimbaji kinara bendi ya Queen ya Uingereza, Freddie Mercury ambaye ni mzaliwa wa visiwani Zanzibar imenyakua tuzo mbili kubwa za tamasha la filamu la Golden Globes.

Tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana huko Beverley Hills, California nchini Marekani ambapo Bohemian Rhapsody imenyakua tuzo katika kipengele cha filamu bora ya mwaka 2018 na Rami Malek ambaye ndiye alikuwa mhusika mkuu akiigiza kama Mercury amenyakua tunzo ya mwigizaji bora wa kiume.

Filamu nyingine zilizoshinda tuzo hiyo ni 'A Star Is Born' ambayo ilipendekezwa sana lakini iliambulia tuzo moja tu. Huku filamu ya Green Book ilikua ni moja kati ya filamu kubwa zilizong'aa baada ya kunyakua tuzo tatu za filamu bora ya kuchekesha, mwigizaji bora msaidizi iliyoenda kwa mwigizaji Mahershala Ali na filamu iliyoandikwa vizuri zaidi.

Ushindi wa Bohemian Rhapsody unakuja kwa kishindo ijapokuwa kulikuwa na vikwazo vingi wakati wa utayarishaji wake.

Muongozaji Mkuu (Director) wa awali wa filamu hiyo Bryan Singer alifukuzwa kazi kutokana na kile kilichotajwa kuwa "tabia zisizovumilika" na kuibua taarifa kuwa alikua na mifarakano na Malek wakati wakiandaa filamu. Dexter Fletcher akaletwa ili kumaliza utayarishaji wa filamu hiyo.

Filamu hiyo imevuma sana na kufanya vizuri katika mauzo sokoni na sasa jina la Malek litaingia katika majina pendekezwa ya tunzo maarufu zaidi za Oscar baadae mwezi huu.

Katika hotuba yake wakati akipokea tunzo hiyo Jumapili usiku, Malek hakumshukuru Singer, lakini badala yake alitoa heshima kwa bendi ya Queen na kusema kuwa amejawa furaha sana kwa ushindi huo.

"Kwako, Brian May, kwako, Roger Taylor, kwa kuhakikisha kwamba uhalali uhalisia unabaki duniani," alisema. Wote May na Taylor ambao ni waasisi wa bendi hiyo walihudhuria sherehe hizo.

Alielekeza tunzo hiyo kwa Mercury, ambaye alifariki mwaka 1991, na kuongeza: "Hii na kwaajili yako na kwasababu yako!"
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FILAMU YA MWANAMUZIKI KUTOKA ZANZIBAR YAZOA TUZO FILAMU YA MWANAMUZIKI KUTOKA ZANZIBAR YAZOA TUZO Reviewed by GEOFREY MASHEL on 1/08/2019 06:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.