Loading...

MSANII MAARUFU WA RAP WA NCHINI KENYA ADAIWA KUMUUA MWANAFUNZI

Loading...
Msanii tajika wa kufoka Oktopizzo anadaiwa kumuuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Strathmore baada ya kumpata katika nyumba yake kwenye mtaa wa Woodley, Kibra.

Henry Ohanga maarufu kama Octopizzo anadaiwa kumuua mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 kwa njia ya kutatanisha.

Kulingana na runinga ya KTN, familia ya mwendazake Kenneth Abom ina uhakika kuwa Octo alihusika katika mauaji ya mwanao ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu. 

Inadaiwa kuwa msanii huyo alimshambulia mwanafunzi huyo kwa panga hadi orofa ya nne kabla ya mwanafunzi huyo kuamua kujirusha chini na kufa baadaye.

Kisa hicho kilifanyika Alhamisi, January 17, msanii huyo akijitokeza kukana vikali madai hayo. 

Kulingana na shahidi, Octo alizozana na mwanafunzi huyo kabla kuanza kumshambulia kwa panga.

''La, sikumpiga kijana huyo. Babake alikuwa mtu wa kwanza niliyezungumza naye baada ya kisa hicho. Nilitaka kujua ni kwanini alikuja katika nyumba yangu. Saa moja baadaye, tulisikia kijana huyo akiangushwa kutoka gorofa ya nne,’’ Octo aliiambia KTN kwa njia ya simu.

Nduguye marehemu, Paul Abom alieleza kuwa Kenneth alifika katika nyumba yao kwenye orofa ya nne huku amejawa damu na jeraha la panga kichwani.

Alilazwa hospitalini kwa siku moja na kufariki Jumamosi, Januari 19, familia yake ikamshtumu Octopizzo kwa kifo chake.
Na Vicky Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MSANII MAARUFU WA RAP WA NCHINI KENYA ADAIWA KUMUUA MWANAFUNZI MSANII MAARUFU WA RAP WA NCHINI KENYA ADAIWA KUMUUA MWANAFUNZI Reviewed by GEOFREY MASHEL on 1/22/2019 08:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.