Loading...

MUIGIZAJI MAARUFU IRINE PAUL AZICHAPA LOCATION

Loading...
Mwanadada Irene paul na Mary mawigi wameripotiwa kupigana wakiwa location walipokuwa wakifanya kazi yao. Wawili hao ambao walikuwa wakiigiza filamu ya  HUBA, walishindwa kuelewana katika baadhi ya mambo na ndipo Irene alipoamua kumsukuma mary na Mary kushindwa kuvumilia na kumpiga vibao  na ndipo varangati lilipoanza.

Wawili hao walishindwa kumaliza tofauti zao na kuamua kuondoka sehemu ya kufanyia kazi kwa muda huo.

Hata hivyo baada ya kutafutwa na kuulizwa kuhusu tetesi hizo, wawili hao kila mmoja kwa nafasi yake alishindwa kutoa majibu ya kueleweka huku mary akishangaa ni nani amevujisha ubuyu huo na kusema wao ni wakubwa wanajua jinsi ya kuyatatua.

Kwa upande wa Irene Paul hakupokea simu ya mwandishi na hata ulipotumwa ujumbe alionekana kuuusoma lakini hakujibu.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MUIGIZAJI MAARUFU IRINE PAUL AZICHAPA LOCATION MUIGIZAJI MAARUFU IRINE PAUL AZICHAPA LOCATION Reviewed by GEOFREY MASHEL on 1/29/2019 07:53:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.