Loading...
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko makubwa ya kifo cha muigizaji nguli wa filamu Bibi. Salome Nonge Maarufu kama Mama Abdul, kilichotokea siku ya Ijumaa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Enzi za uhai wake Bibi. Salome Nonge aliwahi kutamba na kundi la Mambo Hayo miaka 1995, pia amewahi kuigiza filamu mbalimbali ikiwemo Mwantumu na Kigodoro ambazo zilizompatia umaarufu zaidi.
Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa Chama cha Waigizaji Tanzania, tasnia ya filamu, wadau wote wa filamu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwaombea kwa mwenyezi Mungu kuwapo faraja katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.
Na Chama Bernard.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WAZIRI MWAKYEMBE ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA YA MAMA ABDUL
Reviewed by By News Reporter
on
1/28/2019 12:34:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: